JAMII WAMETAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUSOMA VIATBU VYA KISWAHILI ILI KUWEZA KUPATA TAALUMA YA JUU

Wanajamii na Wapenzi wa Lugha ya Kiswahili wametakiwa kuwa na Utamaduni wa Kusoma Viatbu vya kiswahili ili kuweza kupata Taaluma juu ya mambo mbali mabli.

Akisoma Risala Mwenyekiti wa Klabu ya kusoma Vitabu Bi. Maryam Hamdan Amesema lengo la kuanzisa Klabu hiyo ni kuhuisha na kuwahamasisha Wanafunzi na Wanajamii kurejesha Utamaduni wa zamani wa Kusoma Vitabu ambao kwasasa umepotea kutokana na utandawazi.

Bi. Maryam amesema Klabu yao pia inajihusisha na kufanya uhakiki wa Vitabu mbali mbali vikiwemo vilivyomo katika Mitaala ya Wanafunzi  ili kuweza kuwasaidia na kuwajenga Wanafunzi kuwa na Utamaduni wa kupenda kusoma vitabu na kuweza kupata Ufaulu Mzuri katika Masomo yao.

Akizinduwa  Klabu hiyo ya Kusoma Vitabu katika Ukumbi wa Maktaba Kuu Maisara Mjini Magharib Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pembe Juma amesema Wizara ya Elimu inaiunga Mkono Klabu hiyo kwani ni njia moja itakayowawezesha Wanafunzi kutumia muda wao mwingi katika kujishughulisha kutafuta Elimu na kuachana na kushiriki katika mambo maovu.

Mh. Riziki pia amewataka Wanaklabu hao kutumia Vyombo vya Habari katika kuwahamasisha zaidi Wananchi kurejesha Utamaduni wa Kusoma Vitabu ili waweze kuamka zaidi na kuona umuhimu wa kujifunza mengi yatakayoijenga Jamii Kiuchumi, Kiutamaduni na Kijamiii kupitia Vitabu.

Kwa upande wao Wanafunzi walioshiriki katika hafla hiyo wamesema miongoni mwa mambo waliojifunza kupitia uhamasishaji huo ni pamoja na kujenga tabia ya kutumia vizuri muda wao katika kutafuta Taaluma  kupitia vitabu ili waweze  kuchambuwa mambo kwa ufasaha.

Comments are closed.

error: Content is protected !!