KUFUATILIA KWA KINA DAWA ZINAZOWEZA KULETA ATHARI KWA WATUMIZI

Umefika  wakati  wa  kufuatilia  kwa  kina  dawa  zinazoweza  kuleta  athari  kwa  watumizi   ili  kulipatia   ufumbuzi  ikiwa  ni pamoja  na  kujuwa   sababu  za  madhara  yatokanayo  na  dawa  hizo.

Akizungumza  katika  kikao  cha  pamoja  juu  kuanda  muongozo  uaoendana  na  mazingira  ya  Zanzibar   kuhusiana  na  ufuatiliaji  wa  madhara  yatokanayo  na  dawa  chanjo  ,  vifaa tiba   na  dawa  za  asili  uongozi  wa  wakala  wa  chakula  na  dawa  Zanzibar   umesema   upo  katika  matayarisho  ya    kadi  ya  mgonjwa itakayomuorodheshea  dawa  zinazomuathiri  ili  kumrahishia  daktari  katika  kumpatia  tiba  sahihi.

Umesema hali  hiyo  itaenda sambamba  na  utolewaji  wa  elimu  katika  vituo  vya  afya  ili   kuweza  kupokea  taarifa  mbali  mbali  za  athari  zitokanazo  na  dawa  kutoka  kwa  wagonjwa  ili  ziweze  kufanyiwa  uchunguzi  na  zile  zenye  madhara  zaidi  ziweze  kuondolewa  sokoni.

Mratibu  msaidizi  kitengo  shirikishi  ukimwi  homa  ya  ini na  ukoma  ndugu Issa  Abeid  Mussa  amesema   mpango kazi  huo   utatowa  uwiano  sawa   uingizaji  dawa  kanda ya   afrika  mashariki   utaomuwezesha  kila  mhudumu  kufuatilia  muongozo  wa  dawa   kwa  mgonjwa  ili  zisiweze  kumpa  madhara pamoja  na  kuripotiwa  mapema  kwa  dawa  zisizomfaa.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App