MASHEHA NA WANANCHI WANAOSAIDIA KUFICHUA MALI ZA SERIKALI WATAKIWA KUTOA TAARIFA SAHIHI

Masheha na baadhi ya Wananchi wanaosaidia kufichua mali za Serikali wameitaka kamati ya baraza la Mapinduzi inayofuatiali  upatikanaji wa mali hizo kuwapa taarifa ya mapema juu ya  kufanya ukaguzi wa mali za Serikali  ili kuwakusanya watu wenye uelewa wa kutoa taarifa sahihi  wa kuwepo mali hizo .

Wameyasema hayo huko shehia za  finya  na kinyasini wilaya ya wete wakati wakitoa maelezo ya uwepo wa mali za serikali ambazo zimefichwa na kutotambuliwa umiliki wake .

Wamesema wazee na watu wenye uelewa ni muhimu kushirikishwa katika utafutaji huo jambo ambalo litasaidia kupatikana mali hizo kwa urahisi zaidi

Nao wajumbe wa kamati hiyo Mheshimiwa Said Soud Said na Mheshimiwa Juma Ali Khatib wamewapongeza wananchi hayo kwa uzalendo waliuonesha wa kuisadia serikali kuzitambua mali zake ili kuzigawa kwa  wanyonge na kuwasaidia katika  maendeleo yao

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!