MAWAKILI WASIO NA SIFA AMBAO WANAITIA DOSARI SEKTA YA SHERIA NCHINI KUDHIBITIWA

Waziri wa Katiba na Sheria Mh Khamis Juma Mwalim amesema Serikali inakusudia kuwadhibiti Mawakili wasio na sifa ambao wanaitia dosari Sekta ya Sheria Nchini.

Akiwasilisha Mswaada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Mawakili sura ya 28 na kutunga Sheria ya Mawakili na Wakuu wa Viapo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mh Mwalimu amesema Zanzibar imekuwa na idadi kubwa ya Mawakili lakini hawatambuliki Kisheria.

Amefahamisha kuwa lengo la Serikali ni kuondosha kasoro katika utekelezaji wa Sheria hiyo pamoja na kuimarisha uadilifu na utawala wa Sheria katika utekelezaji wa majukumu mbali mbali.

Akiwasilisha maoni ya kamati ya Sheria Utawala bora na Idara Maalum Makamo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Zulfa Mmaka Omar amesema kuumarishwa kwa Mswaada huo kutaiwezesha Jumuiya ya Mawakili Zanzibar kufanya shughuli zake kwa ufanisi zaidi..

Wajumbe wa Baraza hilo wameujadili pamoja na kuupitisha Mswaada huo kwa hatua nyengine ili uwe Sheria kamili.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!