SERIKALI YA TANZANIA NA CHINA ZIMETOA TAMKO LA PAMOJA KUHUSU HALI ZA WATANZANIA WALIOKO NCHINI CHINA

Serikali yaTtanzania na China zimetoa Tamko la pamoja kuhusu hali za Watanzania walioko Nchini China na hatua zinazochukuliwa na Nchi hiyo kukabiliana na Virusi vya Corona.

Akizungumza katika Kikao cha pamoja kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba John Kabudi na Balozi wa China aliyekuwepo Nchini na Waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu amesema mpaka sasa hakuna Mtanzania yeyote au Raia wa Kigeni aliyethibitika kuwa na Virusi hivyo.

Hata hivyo Serikali inaendelea kuchukua hatua stahiki na za dharura ikiwemo kuwapima Watu wote Wanaowasili Nchini kupitia Viwanja vya Ndege na aina nyingine za Usafiri.

Nae Prof.Palamagamba Kabudi Amefahamisha kuwa Ubalozi wa China umeomba fursa ya kukutana na Serikali ya Tanzania kwa nia ya kueleza hali ilivyo Nchini China, hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Nchi hiyo katika kukabiliana na Maradhi hayo na hali ilivyo kwa Watanzania Wanaoishi Nchini China.

Balozi wa China Nchini Wu Ke amewaondoa wasiwasi Watanzania kwa kusema kuwa zaidi ya Wanafunzi 4000 waliokuwepo Nchini China hasa katika Mji wa Wuhan ambao imeathirika na Virusi vya Corona wapo salama na hakuna aliyeathiriwa.

Comments are closed.

error: Content is protected !!