UJENZI WA MTARO WA BARABARA YA MIKUNGUNI UNATARAJIWA KUKAMILIKA MWISHONI WA MWEZI WA TATU MWAKA HUU

Ujenzi wa Mtaro wa Barabara ya Mikunguni unaoendelea kujengwa   unatarajia kutumia kiasi cha Shilingi Bilioni 49 badala ya pesa za awali zilizotarajiwa kutumika Bilioni 23 na kukamilika  kwa Ujenzi huo ni  tarehe 31 mwezi wa tatu  Mwaka huu .

Akitoa Taarifa za Ujenzi wa Mtaro huo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya CRJE  Nd.John Yakuru  ameelezea hali ya Ujenzi  wa Mitaro ya Kilimani na Mikunguni amesema wako katika hatua nzuri nawatakamilisha kwa wakati uliopangiwa  na kuwataka Wananchi kuwa wastahamilivu .

Amesema   wapo katika hatua za mwisho katika Mtaro wa Mikunguni na baadae kurejesha hali ya Barabara kama ilivyokuwa  kwani Barabara hiyo ina kilomita 20  ambapo mradi huo  wa Mitaro unasimamiwa na ZUPS chini ya usimamizi Mkuu Wizara ya Fedha

kwa upande wa Wananchi wanaotumia  Barabara ya Mikunguni pamoja na Wafanya Biashara pembezoni mwa Barabara hiyo wameiomba Serikali kuwasimamia Wakandarasi  wa Ujenzi huo kumaliza kwa haraka ili kuendelea  na harakati zao za maisha  kwa vile  Barabara hiyo  imechukua muda mrefu Ujenzi wake .

Wamesema licha ya kuwa Ujenzi wa Barabara hiyo kuendelea lakini bado imekuwa ni kero kwao  na kuikosesha Serikali Kodi   pamoja na wao kukosa kufanya biashara zao vizuri kwa sababu wateja hawapiti njia hiyo   hivyo basi wameiomba Serikali kuliona hilo ili  kukamilika kwa ujenzi huo kutatoa fursa kwao na kuweza kuendesha  harakati zao za maisha

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!