UMUHIMU WA KUHUDHURIA CLINIC MAPEMA WAKATI WA UJA UZITO.

Wakunga wa kienyeji na wahudumu wa afya wa kujitolea wametakiwa  kuwaelimisha  kina mama umuhimu wa kuhudhuria  clinic  mapema  mara tu baada ya kujigundua kuwa na uja uzito.

Akizungumza  katika mafunzo elekezi  juu ya umuhimu wa clinic kwa akina mama wajawazito kwa wakunga na wahudumu wa afya  wanaojitolea wa wilaya ya kusini katika   kituo cha walimu tc kitogani  diwani wa wadi ya makunduchi  Bi: Zawadi  Hamdu Vuai amesema  kufanya hivyo kutawasaidia kina mama  wajawazito  kuepukana  na matatizo mbali mbali yanayojitokeza hasa wakati wa kujifungua

Ujenzi wa vituo  vya utoaji wa huduma  hizo karibu na  maeneo ya wanachi  itasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na  uzazi.

Mraibu  wa huduma za afya ya mama na mtoto wilaya ya kusini   ndugu Safia  Khamis Juma  amesema  mafunzo hayo yametolewa  baada ya kugundua kina mama wengi kukosa muakmo  wa kuhudhuria clinic wanapokua waja wazito.

Nao wakunga  hao wamesema  licha ya juhudi wanazozichukua  za kuwafikisha kina mama wajawazito  hospitalini kwenda kujifungua  lakini wanakabiliwa na  matatizo mbali mbali ikiwemo kurudishwa  nyumbani kwa wajawazito hao wanapochelewa  kujifungua.

Wilaya ya kusini  ni miongoni mwa wilaya zilofanikiwa  kwa  kuhamasika  kujifungulia hospitali na kufikia asilimia  97  jambo ambalo limepelekea kupungua kwa idadi ya vifo  vitokanavyo na uzazi

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App