UTAFITI ULIOFANYWA NA UNESCO MWAKA 2016 WATAJA ASILIMIA YA WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA

Imebainika kuwa  kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na unesco mwaka 2016  asilimia 20 ya watu wasiojua kusoma na   kuandika  ni miongoni mwao  wakiwa wanawake kwa asilimia 66 ambapo tatizo hilo limeonekana  kuwa  nii kubwa na juhudi za makusudi zinahitajika ili kuondosha tatizo hilo duniani .

Siku ya kujua kusoma na kuandika  huadhimishwa kila ifikapo  tarehe 8/9  na leo siku hiyo imeadhimishwa  kimataifa  katika viwanja vya maktaba kuu  maisara  lengo ni  kuona serikali inachukua juhudi za makusudi  ili kuliondosha kabisa tatizo hilo  kwani kila panapo watu watano mmoja wapo hajui kusoma wala kuandika  .

Mkurugenzi wa maktaba kuu  zanzibar Bi Sichana Hajin Foum ameyasema hayo katika kilele  cha madhimisho hayo kimataifa  amesema kujua kusoma na kuandika ni silaha madhubuti  ambayo  huinua jamii  na hali ya Nchi  ambayo inahamasisha watu  kupata  elimu endelevu  na kuelewa majukumu yao . Na kuihamasisha jamii kupenda kusoma na kuandika  .

Naibu waziri wa elimu mafunzo ya amali Mhe Simai Mohammed Said amesema kuwa serikali imekuwa ikichukuwa juhudi za nmakusudi katika kuhakikisha wananchi wake wana soma na kupata elimu inayostahiki ili kujenga taifa bora na lenye wasomi . Amesema mashirikiano yapamoja yanahitaji kwa walimu na wazazi .

mapema naibu waziri alikagua maktaba ya watoto  na kuangalia maendeleo    ya maktabaa hizo na kuitaka  jamii kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu pamoja na wazazi  na skuli kuzitumia maktaba hizo kwa manufaa  yao.

nao wadau wa jumuia ya wakutubi  wakaipongeza  serikali kutokana na mashirikiano ya pamoja katika kushajihisha  jamii na kutoa elimu mbalimbali kwa wakutubi.

Comments are closed.

error: Content is protected !!