UWT ITAENDELEZA KASI YA KUTAFUTA WANACHAMA WAPYA ILI KUIMARISHA JUMUIYA HIYO

Naibu Katibu Mkuu wa UWT  Zanzibar Nd.Tunu Juma Kondo amesema Jumuiya hiyo itaendeleza kasi ya kutafuta Wanachama wapya ili kuimarisha Jumuiya hiyo na Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza na Wanachama wa UWT  Mkoa wa Kusini Unguja huko Dunga pamoja na kukabidi kadi Wanachama wapya Nd.Tunu amesema Jumuiya za Chama ni chachu za kuimarisha CCM  hivyo hazitasita kuandikisha Wanachama wapya  ili kukipa nguvu zaidi.

Amesema UWT  itaendeleza juhudi za malezi bora ya Watoto  wa Tanzania wakuwe katika maadili mazuri ili baadae wawe Viongozi waadilifu.

Mwakilishi wa viti maalum Mkoa wa Kusini Unguja Mh.Wanu Hafidh Ameir amesema Viongozi wa Mkoa huo wataongeza juhudi za kuwawezesha Vijana kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo vyarahani ili waweze  kujikwamue na umasikini .

Katibu wa CCM  Jimbo la Tunguu Nd.Sharifa Maabad Othaman amesema Jumuiya ya UWT  Mkoa  Kusini imefanikiwa kutekeleza kazi zake vizuri lakini pia inakabiliwa na tatizo la Wanachama kutolipa ada sambamba  na vikiundi vya Kinamama kuwa na mitaji midogo ya kuendesha miradi yao.

Mkutano huo ni sehemu ya maadhimisho ya kutimia miaka arobaini na tatu ya kuanzishwa Chama Cha Mapinduzi

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!