WAJASIRIAMALI WA MATUNDA NA MBOGA MBOGA KISIWANI PEMBA WAMETAKIWA KUZALISHA KWA WINGI BIDHAA ZAO

Wajasiriamali wa matunda na mboga mboga kisiwani Pemba wametakiwa kuzalisha kwa wingi bidhaa zao pamoja na kuzalisha bidhaa zilizo bora ili kuyafikia masoko ya ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa na kaimu Afisa Mdhamin Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee  Wanawake na Watoto Hakimu Vuai Shein huko Gombani wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya awali kabla ya kupewa mikopo kwa wajasiri amali hao

Kwa upande wake kaimu mratibu  mfuko wa uwezeshaji Haji Khamis Haji amesema Mfuko huo unalengo la kuwawezesha wananchi wake hasa kipato cha chini pamoja na  kuwataka fedha hizo waweze kuzirudisha kama walivyopangiwa

Nao wajasiri amali hao wamesema watahakikisha watayatumia taaluma  waliyopewa  ili waweze kufikia malengo yao .

Jumla ya sh millioni ishirini zinatarajiwa kutolewa kwa wajasiri amali thalathini na tisa wakiwemo wanawake kumi na saba na wanaume ishirini na mbili.

Comments are closed.

error: Content is protected !!