WANANCHI WA ZANZIBAR WAMETAKIWA KUYALINDA MAPINDUZI YAO KWA KUHAKIKISHA CCM INABAKI MADARAKANI

Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewataka Wananchi wa Zanzibar kuyalinda Mapinduzi yao kwa kuhakikisha CCM inabaki Madarakani kila unapofanyika Uchaguzi.

Spika ameeleza hayo katika Hafla ya kuweka  Jiwe la Msingi la Tawi la CCM  Mwera  Kiongoni  eneo alilozaliwa Muasisi wa Mapinduzi  ya Zanzibar hayati Abeid Amani Karume na Mkutano  wa  Wana CCM uliofanyika Ukumbi wa Dr, Ali Mohammed Shein  huko Tunguu.

Amesema kuiondoa  CCM  Madarakani ni sawa na kuyakataa Mapinduzi na matunda yake ikiwemo Elimu bure na Afya.

Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mh. Ayoub Mohammed Mahamoud amewataka Wana  CCM  wa Mkoa huo kuendeleza sira ya Mkoa wa Kusini kuwa ni Ngome ya CCM.

Katika hatua nyingine Chama cha  Mapinduzi  Wilaya  Mjini kimefanya zoezi la kupandisha Bendera katika Nyumba za Mabalozi wake wa Jimbo la Raha Leo kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 43 ya Kuzaliwa   Chama hicho na kujipanga kuukabili Uchaguzi  Mkuu wa Mwaka  huu.

Comments are closed.

error: Content is protected !!