WATOTO WAHAMASISHWA KUSHIRIKI CHEMSHA BONGO ZA DINI YA KIISLAM

Wazazi na walezi wametakiwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki kikamilifu katika kujibu masuali mbalimbali ya dini ya kiislamu kwa lengo la kuijua kwa undani dini yao.

Wito huo umetolewa na naibu katibu mkuu anaeshughulikia habari katika wizara ya habari utalii na mambo ya kale Shekhe Saleh Yussuf Mnemo katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa chemsha bongo ya ramadhani.

Shekhe Mnemo amesema kipindi cha chemsha bongo ya ramadhani ni chachu ya kuwakumbusha watoto na waislamu kwa ujumla kuifahamu na kuielewa vyema dini ya kiislam.

Nao wafadhili wa kipindi hicho wamewataka watayarishaji wa kipindi hicho kuandaa utaratibu wa kipindi hicho kuonyeshwa ZBC TV.

Akisoma risala ya watayarishaji wa vipindi vya ramadhani Zanzibar Bi Aziza Hassan amesema kipindi hicho kina changamoto nyingi ikiwemo kukosa wafadhili wa kutosha ili   kuwapatia zawadi washindi.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App