WAZEE, WALEZI PAMOJA NA WADAU WA MICHEZO WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA

Wazee, walezi pamoja na wadau wa michezo   wametakiwa kushirikiana kuibua vipaji vya vijana vilivyojificha katika michezo hasa maeneo ya vijini kwani  michezo imekuwa ikitoa fursa nzuri ya ajira  na kujikwamua kiuchumi.

Wito huyo umetolewa na mjumbe wa NEC Taifa nd Ramadhani Shaibu Juma  wakati alipokuwa akikabidhi vifa vya michezo na kusherekea ushindi kwa  timu ya fast fast ya  kangangani iliyoibuka na ubingwa katika  kombe la kangangani cup.

Amesema michezo ni ajira endapo vijana hao wataendelezawa vizuri kwa  kutumia vipaji vyao wanaweza kujiri wenyewe kupitia michezo na kuendeleza utamaduni.

Mapema afisa kitengo cha uratibu chama chama pinduzi ccm pemba   mabaye pia ni mlezi wa timu hiyo zulefa abdall said ameipongeza timu ya fasta fast kwa haraka zao za kukimbilia ubingwa kama lilivyo  jina lao    kwa kupata ubingwa huo  kwani mbio za sakafuni hazikuishia ukingoni.

Nao wanachezo wa timu hiyo wamesema licha ya kuibuka na ubingwa huyo ila bado wanakabiliwa na changamoto  mbali mbali ikiwemo ya vifa vya  michezo.

Comments are closed.

error: Content is protected !!