WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MH. MWALIMU AMETOA TAARIFA YA MAADHIMISHO WIKI YA MSAADA WA KISHERIA

Waziri wa Katiba na Sheria  Mh.Khamis Juma Mwalimu Ametoa Taarifa juu ya  Maadhimisho ya wiki ya msaada wa Kisheria ambayo itaenda sambamba na siku ya Sheria kwa mwaka 2020 itakayo fanyika siku ya Ijumaa Tarehe 7 Mwezi huu.

Akizungumza  katika Mkutano na Waandishi  wa Habari  uliofanyika  katika Ukumbi wa Ofisi ya katiba na Sheria Mazizini  amesema maadhimisho hayo  yatajumuisha  shughuli mbalimbali  kwa Unguja na Pemba ikiwemo utoaji wa Elimu  kwa Wananchi kupitia Vyombo vya Habari ikiwemo Redio na Televisheni, Ziara katika Shehia mbali mbali ili kuwapatia Wananchi Elimu ya Msaada wa Sheria katika Maeneo yao.

Amesema lengo la kutoa Elimu hiyo ni kuwawezesha Wananchi kufahamu haki zao za sheria ambazo zitattua kero zinazo wakabili na kufikia mahitaji ya kuundwa kwa sheria hizo.

Maadhimisho hayo pia yataambatana na shughuli kuu mbili ambazo ni Uzinduzi  wa  usajili wawatoa Huduma za Msaada wa kisheria kwa njia ya Kielekroniki na pia Uzinduzi wa Sheria ya Msaada wa Kisheria kwa Lugha nyepesi.

Kauli  mbiu ya maadhimisho hayo ni upatikanaji wa msaada wa kisheria ni nguzo kwa Ustawi wa Jamii ikiwa lengo kuu ni kuona Ustawi wa Jamii unaimalika kupitia msaada huo wa Kisheria.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!