WENYE VITUO VYA KUHIFADHIA MITUNGI YA GESI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA USALAMA

Naibu mkurugenzi wa kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar Nd: muhidini ali muhidini amewataka wenye vituo vya kuhifadhia mitungi ya gesi na maduka ya kuuzia gesi kufuata taratibu za kuweka vifaa vya usalama katika maduka yao ili kuepuka maafa.

Akizungumza mara baada ya kukagua vituo vya kuhifadhia mitungi ya gesi vya kisiwandui na mtoni mkurugenzi huyo amesema ni vyema wenye vituo vya kuhifadhia mitungi ya gesi kuzingatia usalama wao na wateja kwa ujumla ili kunusuru maafa kutokea.

Taifa ges Tanzania limited na ges energe ambao walitembelewa na kamisheni hiyo wamehaidi kuyatekeleza kwa kurekebisha mapungufu yote yaliyokuwemo kwenye vituo hivyo.

Ukaguzi huo utaendelea kufanywa na kamisheni hiyo katika maeneo mbalimbali hapa zanzibar ili wananchi waweze kuelewa na kuweza kuepuka na maafa ambayo yanaweza kuepukika.

Comments are closed.

error: Content is protected !!