WIZARA YA AFYA IMEZINDUA MPANGO WA AFYA YA JAMII UTAKAOTOA HUDUMA ZA AFYA KWA HATUA ZA AWALI

Wizara ya Afya imezindua mpango waAfya ya Jamii utakaotoa huduma za Afya kwa hatua za awali kwa Mtu mmoja mmoja katika ngazi ya Shehia ambao utarahisisha mfumo wa kutoa huduma bora za Afya kwa Wananchi

Mpango huo umezinduliwa na Waziri wa Biashara naViwanda Balozi Amina Salum Ali katika Mkutano wa Mwaka wa Wizara hiyo uliowakutanisha Wadau wa Sekta ya Afya, Taasisi naWashirika wa Maendeleo.

Wakizungumza katika Mkutano huo Balozi Amina na Waziri wa AfyaMh. Hamad Rashid Mohamed wamesema mpango huo ni  kutimiza Sera ya Serikali ya kutoa huduma za Afya bure ambapo Zanzibar ipo katika nafasi nzuri kwa Nchi nyingi za Afrika kuwafikia Wananchi wengi hasa wa Vijijini.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay amesema Wizara ya Afya inapaswa kufanya juhudi za kukabiliana na matatizo ya vifo vya Mama na Mtoto na maradhi yasiyoambukiza na pia kutoa huduma bora za Afya zinazoendana na Sera za WHO

Mkutano huo wa 15 wa kutathmini utoaji wa huduma, matatizo na mapendekezo kwa Mwaka ujayo umeelezea mafanikio yaliyofikiwa na Wizara hiyo ikiwemo kuongeza idadi ya Madaktari kutoka Daktari mmoja kwa Wagonjwa 31, 838 Mwaka 2010 hadi kufikia Daktari 1 kwa Wagonjwa 6,276 2019.

Comments are closed.

error: Content is protected !!