ZAC IMESEMA IMEBAINI KUPUNGUA HOFU YA JAMII KUHUSU MAAMBUKIZI YA VIRUSI VINAVYOSABABISHA UKIMWI

Tume ya ukimwi Zanzibar, ZAC imesema imebaini kupungua hofu ya jamii kuhusu maambukizi ya Virusi vinavyoasababisha Ukimwi licha ya juhudi kadhaa kuchukuliwa.

Akitoa taarifa ya kuhusina na hali ya maambuziki ya Ukimwi Zanzibar Mkurugenzi wa tume hiyo Ahmed Mohamed Khatib, amesema matatizo hayo yamechangia baadhi ya vijana kudharau njia za kujikinga na viashiria vya inavyosababisha  kupata maambukizo  hayo.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi ARV, ameiomba Serikali kutenga bajeti maalum ya kununulia dawa hizo, ili kuepusha utegemezi wa wafadhili kutoka nje ya nchi.

Mwenyekiti wa kamati  hiyo, mh Bi Panya Ali Abdallah, ameiomba serikali kutoa ushirikiano zaidi na tume hiyo ili kila mmoja ajue kuwa ukimwi  upo na unaoendelea kuathiri.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!